Simba Savings - Kupokea TZS 900,000

KIASI CHA KUPOKEA
TZS 900,000
IDADI YA SIKU ZA MCHEZO
SIKU 30
ADA YA KIJUMBE
TZS 1,000
Kwa muda mrefu, watu walitumia njia hii kuu:
- ○ Kuhifadhi nyumbani – rahisi lakini hatarishi kutokana na wizi, dharura au matumizi yasiyopangwa.
Suluhisho
ShinePortal Microfinance tumekuja na huduma mpya ya kuweka akiba (Savings) kwa mfumo wa kisasa wa mchezo wa kuinuana kiuchumi. Huu ni mfumo wa kipekee unaochanganya ushirikiano, nidhamu na furaha.
Mfumo huu unawasaidia kujiwekea akiba kidogo kidogo kwa njia rahisi, yakuaminika na yenye furaha, huku ukijenga ushirikiano kati ya washiriki.
Hii siyo tu kuweka akiba – bali ni harakati ya kuinuana kiuchumi kwa pamoja
Kwa nini uchague sisi?
Huduma yetu si tu njia ya kuweka akiba, bali ni njia ya kisasa ya kujenga jamii yenye nguvu za kiuchumi. Hakuna urasimu, hakuna hofu ya wizi nyumbani, na kila mmoja anafaidika.
Usalama Wa Fedha Zako
Katika Mchezo wa Kuinuana Kiuchumi, usalama wa fedha za washiriki ni kipaumbele chetu. Tumetengeneza mfumo thabiti unaohakikisha kila mshiriki anapokea malipo yake bila kusumbuka, hata kama kutatokea changamoto kama mchezaji kujitoa, kuchelewa kuchangia, au hata kufariki dunia.
Jinsi Tunavyohakikisha Usalama Wa Malipo
-
Mfumo Imara
- ● Mchezo huu unasimamiwa na ShinePortal Microfinance kwa uwazi na uangalizi wa hali ya juu.
-
Nafasi Zinazokamilishwa
- ● Ikiwa mshiriki mmoja atajitoa au hatoweza kuendelea, kampuni itachukua nafasi yake kwa muda ili kuhakikisha kuwa mzunguko hauathiriki.
-
Hakuna Hasara kwa Washiriki
- ● Washiriki wote waliobaki wataendelea kupokea malipo yao kama kawaida bila kuathirika.
-
Mfumo wa Akiba
- ● Kuna akiba ya dharura inayotumika kuhakikisha mzunguko wa malipo unaendelea hata katika hali zisizotarajiwa.
Uhakika Wa Malipo,
Kwa mfumo huu thabiti:
- Kila mshiriki anapokea malipo yake kwa wakati bila kuchelewa.
- Hakuna anayepoteza fedha zake, hata kama mshiriki mwingine atajitoa.
- Kampuni inasimamia kila hatua kuhakikisha uwazi na uaminifu.
- Kwa hivyo, unaweza kushiriki bila hofu na kufurahia faida za mshikamano wa kifedha!
Faida za Kushiriki
- Uwezo wa kupata mkopo wa fedha wa hadi TZS 1,000,000 bila dhamana ambapo mchezo ndio utakaotumika kama dhamana
- Unakusaidia kuweka akiba kwa njia ya mshikamano.
- Unapata pesa zako kwa wakati na bila usumbufu.
- Unajenga mtandao wa kifedha na watu waaminifu.
- Mfumo ni rahisi na hauna masharti magumu.
Jinsi Mfumo Unavyofanya Kazi
- Kila mshiriki anachangia kiasi husika cha aina ya mchezo anaoshiriki
- Washiriki hupokezana kupokea malipo ya mchezo kulingana na mpangilio wa mzunguko.
- Malipo yanafanyika kwa uwazi na haki kwa kila mshiriki.
- Mfumo huu unakuza nidhamu ya kifedha na kusaidia kushughulikia mahitaji ya haraka.
Sifa Za Kushiriki
-
Umri
- ● Kuanzia miaka 18 na kuendelea.
-
Usajili
- ● Kila mshiriki lazima ajisajili rasmi kwenye tovuti yetu na kutuma maombi ya kujiunga na mchezo huu kabla ya kuanza.
-
Uaminifu
- ● Ni lazima kila mshiriki awe mwaminifu na aelewe umuhimu wa mchango wa kila siku.
Vigezo Na Masharti
-
Ushiriki
- (a) Mchezaji lazima ajisajili rasmi na kukubali vigezo na masharti haya kabla ya kushiriki.
- (b) Kila mshiriki atatakiwa kuchangia kiasi kilichopangwa ili kuendelea kwenye mchezo.
-
Kujitoa
- (c) Mshiriki anayeamua kujitoa kabla ya kukamilisha mzunguko wake atarudishiwa 50% ya kiasi alichochangia.
- (d) Hakuna marejesho ya zaidi ya nusu ya mchango wa awali kwa wanaojitoa njiani.
-
Muda wa Kutoa
- (e) Mshiriki anatakiwa kutoa mchango wake kwa wakati uliopangwa.
- (f) Kushindwa kutoa kwa muda muafaka kutasababisha faini ya 10% ya kiasi anachotakiwa kutoa.
-
Uwazi na Uadilifu
- (g) Washiriki wanapaswa kuwa waaminifu na kufuata utaratibu bila kufanya udanganyifu.
- (h) Mchezaji yeyote atakayebainika kufanya udanganyifu atafukuzwa kwenye mchezo bila kurejeshewa mchango wake.
-
Mawasiliano
- (i) Mshiriki anawajibika kuwasiliana na waandaaji wa mchezo huu kwa matatizo yoyote yanayoweza kujitokeza.
- (j) Kutozingatia mawasiliano kunaweza kuathiri haki ya mchezaji kwenye mchezo.
Ada Ya Kijumbe
Ni TZS 1,000 tu!