Unajua waajiri wanapenda kuona nini kwenye CV yako? Leo tunakuletea vidokezo muhimu vya kuandika CV...Read more
Nini Hasa Tofauti Kati Ya CV na RESUME
- By Admin
- 17 - April - 2024
Nini hasa ni tofauti kati ya CV (wasifu wa kitaaluma) na Resume (maelezo binafsi)?
Ingawa mara nyingi tunatumia maneno haya kwa kubadilishana, kuna tofauti mkubwa hasa katika muundo na kusudi lao.
Tuangalie kwa undani:
1. CV inaweza kuwa na ukurasa nyingi na huonyesha elimu yako yote, uzoefu wa kazi, ustadi, miradi iliyofanikiwa na mafanikio yanayohusiana na kazi.
Resume kwa kawaida ni ukurasa mmoja au mbili na inalenga kuvutia mwajiri kwa kutoa maelezo ya kipekee, ujuzi, na uzoefu unaofaa.
2. CV ina lengo la kutoa maelezo mazito na kamili kuhusu historia yako ya kitaaluma.
Resume ni muhtasari mfupi unaolenga zaidi kwenye habari muhimu na inayohusiana na nafasi unayotafuta.
3. CV inapaswa kuzingatia tarehe za kazi zilizopita, elimu na inaweza kujumuisha sehemu kama vile "Wasifu wa Kitaaluma," "Elimu," "Uzoefu" "Ustadi na Maarifa," n.k
Resume kwa kawaida ina sehemu kama vile "Muhtasari wa Kazi," "Ustadi Muhimu," "Elimu," na "Mafanikio ya Kazi."
Kwa kumaliza,
CV nzuri inazingatia habari yako ya kitaaluma kwa kina na inaweza kuwa ndefu.
Resume ni muhtasari mfupi zaidi ambao unalenga kumvutia mwajiri na kuonyesha ujuzi na uzoefu unaofaa kwa nafasi hiyo maalum.