Unajua waajiri wanapenda kuona nini kwenye CV yako? Leo tunakuletea vidokezo muhimu vya kuandika CV...Read more
SALARY NEGOTIATION
- By Admin
- 17 - April - 2024
SALARY NEGOTIATION!
Kujadiliana mshahara wako ni sehemu ya kawaida kwenye mchakato wa ajira.
Waajiri wanatarajia hivyo na ni fursa ya kuonyesha ujasiri, ujuzi na thamani utakayotoa kwenye kampuni yao.
Hizi ni TIPS kuhakikisha unapata mkataba wa mshahara utakao ridhika nayo:-
1. Muda ni Muhimu:
Wakati bora wa kujadiliana mshahara wako ni baada ya kupokea ofa ya kazi na sio kabla.
Ikiwa tayari una kazi na unaamini unastahili nyongeza ya mshahara, panga mkutano na meneja wako kujadili jambo hilo kwa njia isiyo ya kukinzana.
2. Kuwa na Ujasiri ila Usijione una haki (Entitlement):
Kuwa mnyenyekevu na mchangamfu.
Eleza nia yako ya kuwa sehemu ya timu na ahadi yako ya kutoa matokeo bora kwa ujasiri bila kujiona una haki.
3. Thibitisha Thamani Yako:
Kabla ya kuingia kwenye majadiliano ya mshahara, ni muhimu kufanya utafiti na kuelewa thamani ya soko ya ujuzi na uzoefu wako.
Kuwa tayari kuelezea thamani yako na jinsi itakavyosaidia kampuni.
4. Epuka kutumia hisia:
Kumbuka pande zote mbili zinataka kufikia makubaliano yanayofaa.
Kwa hiyo, kuwa mvumilivu na mwenye heshima wakati wote wa mchakato.
5. Jiwekee Kiwango Cha Chini:
Weka wazi kiwango cha chini cha mshahara kinachokubalika kwako.
Hii itakusaidia kuzingatia lengo.
Hata hivyo, kumbuka kuwa ukaidi uliopitiliza unaweza kutokuwa na matokeo mazuri wakati wa majadiliano.
Kumalizia,
Kujadiliana kuhusu mshahara ni pamoja na kuzugumza kuhusu faida, bonasi, chaguo la hisa, siku za likizo na manufaa mengine.
Muajiri anaweza ana uwezo mdogo wa kukulipa ila mnaweza kukubaliana kama utafikishe target zake, wakufikirie kwenye bonasi n.k
All the best.