Unajua waajiri wanapenda kuona nini kwenye CV yako? Leo tunakuletea vidokezo muhimu vya kuandika CV...Read more
Unapoandaa CV Yako Hebu Jaribu Kuifanya Iwe Fupi Na Ivutie.
- By Admin
- 17 - April - 2024
Unapoandaa CV yako, fanya iwe fupi na ivutie.
Ifikirie kama vile ni hadithi unayomuahadithia muajiri mtarajiwa kuhusu ujuzi wako. Hiyo ndio tiketi yako ya kuajiriwa.
Tumekuorodhesha baadhi ya VIPENGELE muhimu usisahau kuweka ili kupata CV inayoeleweka na yenye ufanisi:
1. Maelezo ya Mawasiliano (Contact Information):
Anza kwa kuandika
- Jina lako
- Nambari ya simu
- Anwani ya barua pepe
- Eneo lako
2. Muhtasari/Lengo:
Andika kwa ufupi malengo yako ya kazi, na utakachochangia.
Hakikisha kila unapo apply kazi mpya unabadilisha Muhtasari kulingana na kazi maalum unayoomba.
3. Uzoefu:
Orodhesha historia yako ya kazi kwa mpangilio wa nyuma kwenda mbele (kazi ya hivi karibuni kwanza).
Jumuisha
- Majina ya kazi
- Majina ya kampuni
- Tarehe
- Maelezo ya majukumu yako na mafanikio
4. Elimu:
Weka taarifa kuhusu historia yako ya elimu, ikiwa ni pamoja na
- Shahada ulizopata
- Taasisi ulizohudhuria
- Tarehe za kuhitimu.
- Taja heshima au tuzo zinazofaa
5. Ujuzi:
Panga kwa makundi.
Onyesha
- Ujuzi wako wa kiufundi (Technical Skills)
- Ujuzi laini (Soft Skills)
- Ujuzi unaoweza Kuhamishika (Transferrable Skills)
6. Vyeti na Mafunzo:
Ikiwa una vyeti au programu za mafunzo zinazofaa, orodhesha hapa.
Vitaongeza imani kwa ujuzi wako.
7. Lugha na Ufanisi:
Thibitisha lugha unazozijua, pamoja na kiwango chako cha ufanisi.
Kwa mfano, fasaha, kiwango cha kati.
Hii ni muhimu hasa kwa fursa za kimataifa.
8. Kazi ya Kujitolea:
Hii inaonyesha uaminifu na tabia yako.
Hakikisha unataja uzoefu wowote wa kazi ya kujitolea unaopatana na kazi unayoomba.
9. Referees:
Ni kawaida kuandika "Marejeleo yanapatikana kwa ombi." (References available upon request)
Ila kama kazi inahitaji uweke Referees, waweke.
10. Mpangilio safi
Tumia:
- Alama za risasi (Bullet Points)
- Vichwa vya habari (Headings)