ShinePortal Agents (60)
- Dead Line: 2025-12-31
ShinePortal inatafuta watu wenye bidii, uwajibikaji na uelewa wa teknolojia za kisasa kufanya kazi kama wakala wa kusajili wateja kwa njia ya mtandao.
Nafasi
Wakala Wa Kusajili Wateja
Idadi
60
Kampuni
ShinePortal
Eneo la kazi
Tanzania
Faida za kuwa Wakala
- Mshahara: TZS 500,000 kwa mwezi
- Mkopo: TZS 150,000 kwa wakala mpya ili kukabiliana changamoto za kifedha za mwanzo kama kununua mahitaji ya msingi, usafiri, au vifaa vya kazi.
- Posho: TZS 3,500 kwa siku
- Fursa ya kukuza kipato na kuendeleza taaluma ndani ya kampuni.
- Mazingira bora ya kazi na msaada wa timu ya ShinePortal.
Sifa Za Mwombaji
- Waombaji wanapaswa kuwa na angalau elimu ya Kidato cha Nne (Form 4) au zaidi.
- Uwezo mzuri wa mawasiliano kwa Kiswahili (Kiingereza ni nyongeza).
- Nidhamu, uaminifu, bidii na uwezo wa kushirikiana na watu.
- Uwezo wa kufanya kazi kwa malengo (target-based).
- Uzoefu katika kazi za mauzo au huduma kwa wateja ni faida lakini sio sharti.
Majukumu Ya Kazi
Kama mfanyakazi wa ShinePortal utawajibika kwa:
- Kusaidia wateja kujiandikisha kwenye mfumo wa kampuni.
- Kuthibitisha malipo ya wateja kabla ya kuanzisha akaunti zao.
- Kutoa ufafanuzi kuhusu mchakato wa usajili.
- Kufuatilia wateja kutimiza malipo na usajili.
- Kutoa msaada kwa wateja wakati wa kujiandikisha.
- Kutoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na kampuni.
- Kuwashauri wateja kwenye huduma zinazofaa kulingana na mahitaji yao.
- Kufuatilia mchakato wa usajili kwa wakati.
- Kusimamia na kuhifadhi taarifa za wateja kwa usalama.
- Kuhamasisha wateja kufanya manunuzi na kulipia huduma.
Mshahara
- Mshahara wa msingi ni TZS 500,000 kwa mwezi
- Mshahara huu unajumuisha bonasi na/au posho kwa kuzingatia uzoefu na ujuzi wa mwombaji pamoja na kiwango cha matokeo ya kazi kama itakavyoainishwa kwenye mkataba rasmi wa ajira
Kama unadhani una sifa zinazohitajika, chukua hatua sasa.
Tuma maombi yako kwa kubofya neno apply now hapa chini ili uwe miongoni mwao watakaoajiriwa ndani ya mwezi huu