ShinePortal Startup Fund

Je, una wazo la biashara lakini huna mtaji wa kuanzisha? Hii ni nafasi yako!
Tunafuraha kukutangazia fursa maalum kwa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 22 hadi 35 ambao wana mawazo bunifu ya biashara lakini wanakabiliwa na changamoto ya mtaji.
Kupitia mpango huu, tunatoa nafasi kwa vijana kushiriki kwenye challage yetu ya ShinePortal Startup Fund, ambapo washiriki watawasilisha mawazo yao ya biashara kwa lengo la kushinda mtaji wa TZS 2,000,000 kila mmoja.
Vigezo vya ushiriki
- Umri kati ya miaka 22 hadi 35.
- Awe na wazo bunifu la biashara linaloweza kuleta mabadiliko chanya kiuchumi.
- Kila mshiriki atatakiwa kulipia ada ya usajili
- Washiriki wote watawasilisha maelezo ya wazo lao kwa mfumo utakaotolewa baada ya kujisajili.
Malengo ya challenge
- Kuwezesha vijana kuingia rasmi kwenye ujasiriamali.
- Kuchochea mawazo ya kibunifu kutoka kwa vijana wa kawaida.
- Kuwapunguzia vijana changamoto ya mitaji isiyopatikana kirahisi.
Zawadi
Washindi walioteuliwa kwa ubunifu, uhalisia na utekelezekaji wa wazo lao watawezeshwa kwa mtaji wa TZS 2,000,000 kwa kila mmoja kutoka kwa investors wetu.
Washindi watapata pia nafasi ya kushauriwa kitaalamu kuhusu uanzishaji na uendeshaji wa biashara zao.
Kumbuka kuwa kwenye shindano letu, kila mshiriki ni mshindi kwa namna yake. Hata kama hutopata nafasi ya kushinda mtaji, bado utaendelea kunufaika kupitia fursa hizi:
- Mafunzo ya Bure – Utapata elimu ya kipekee ya jinsi ya kuendeleza na kutekeleza wazo lako la biashara.
- Ushauri wa Kitaalamu – Washiriki wote watapata ushauri kutoka kwa wataalamu wa biashara na wajasiriamali waliobobea.
- Mtandao (Networking) – Utakutana na vijana wengine wenye mawazo ya biashara na wadau mbalimbali, jambo litakalokupa nafasi ya kushirikiana na kujifunza.
- Fursa za Uhusiano wa Kibiashara – Baadhi ya wadau na taasisi zinazoshirikiana nasi huenda wakavutiwa na wazo lako hata kama hukupata mtaji.
- Kukutana na Wawekezaji – Utapata nafasi ya kuwasilisha wazo lako mbele ya wawekezaji wengine ambao wanaweza kuvutiwa na kulifadhili moja kwa moja.
- Vyeti vya Ushiriki – Washiriki wote watapewa cheti cha kutambua jitihada zao na kujitokeza kushiriki.
- Motisha na Uwezo Mpya – Kupitia mafunzo na ushauri, utajipatia maarifa na kujiamini zaidi kutafuta njia nyingine za kufanikisha ndoto zako.
- Kutambulika – Kupitia shindano hili, jina lako na wazo lako vitafika mbali zaidi, jambo linaloweza kufungua milango mipya ya fursa.
Kwa hiyo, kushiriki pekee ni hatua kubwa ya mafanikio. Shindano hili sio tu kuhusu kushinda mtaji – bali ni kuhusu kukuza maarifa, mitandao, kutambulika na kufanikisha ndoto zako za kibiashara.
Gharama za ushiriki
Kila mshiriki wa shindano anatakiwa kulipia TZS 1,000 pekee kama gharama ya fomu ya ushiriki.
Malipo haya ni hatua ya awali ya kuthibitisha nafasi yako, kabla ya kujaza fomu na kuendelea na mchakato wa kuwasilisha wazo la biashara.
Usajili wa awamu ya pili umeanza rasmi tarehe 23 Septemba 2025 na utafungwa tarehe 23 November 2025. Hakikisha unawasilisha wazo lako mapema.
Changamoto ni fursa kwa wenye ndoto — Shine Your Idea Now!
Tazama Jinsi Mtaji Wa TZS 2,000,000 Ulivyobadilisha Maisha Yao

Kutoka Dodoma

Kutoka Mwanza

Kutoka Arusha